SIRI YA WOKOVU 1

 Warumi 7:1  

Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?

Ndugu zangu hamjui ya kua sheria inamtawala mtu akiwa hai

Warumi 7:2 

Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.


Anasema mwanamke akiwa ameolewa na mwanaume kuna sheria inayowafunga
Mwanamke huyu akienda kwa mme mwingine wakati mme wako bado yu hai basi atakua amevunja sheria

Lakini mume anapokufa huyu mwanamke ile sheria haimfungi tena

Sasa utaona jinsi sheria ilivofanya kazi kwamba bila kifo sheria ilimtawala mkee

Warumi 7:3 

Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.


Sasa mume akiwa hai
Huyu mke akienda kwa mme mwingine ni mzinzi kwasababu ya ile sheria
Lakini anapokufa mme automatic na ile sheria inakua haina nguvu hivo anaruhusiwa kwenda kwa mme mwingine na hatoitwa mzinzi

Sasa Mungu anatufundisha nini kupitia mfano huo

Warumi 7:4 

Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.

Natamani ukiwa unasoma biblia ujifunze kuelewa fact

Kuna watu husoma neno afu wanasema tuombe Mungu atupe kuifia toratii
Nooo mnakoseaa sanaa

Hapa paulo hasemi kwamba kadhalika ninyi mkiomba mtaifia dhambi
Anasema kadhalika ninyi pia mmeifia dhambi yani ni kitu ambacho tayari kimefanyika

Anakuonyesha uhalisia wa jinsi ulivyo

Wakristo wengi wamekua wakimsumbua Mungu kwa kumuomba vitu ambavo tayari wanavyo

Unaposoma neno la Mungu jifunze kutofautisha
Kati ya wakati uliopita
Wakati uliopo
Na wakati ujao
Hizo ni muhimu sana kujua kutofautisha kwenye neno kua kipi ni ahadi na kipi tayari unacho

Sasa hapa anakwambia kitu ambacho unacho tayari wewe hapo unatakiwa sasa uishi katika kukiri hiki kilichosemwa hapa

Anasema kadhalika ninyi pia mmeifia torati

Utasema nimeifiaje wakati nipo hai

Well umeifia kwa njia ya mwili wa Kristo
Kwasababu Yesu alikufa kwa niaba yako
Anasema mmekufa kwa njia ya mwili wa Kristo
Mpate kua mali ya mwingine
Ooh ooh nipate kua mali ya mwingine?
Kwani mwanzo nilikua mali ya nani?

Mwanzo nilikua mali ya shetani ndio maana biblia inasema mmenunuliwa kwa damu ya thamani
Ina maana kuna biashara inayoendelea
Mungu anabiashara na biashara ya Mungu ni kununua watu kupitia damu ya Yesu waje kwake
Kuleta watu kwa Yesu ni kufanya biashara ya Mungu kukua
Kwahio huwezi kua mali ya Yesu kama hujaifia torati
Kwasababu anasema mmeifia torati ili mpate kua mali ya mwingine

Ukweli huu unatakiwa uzame ndani yako
Huwezi kua mali ya Yesu kama hujaifia torati

Afu anamalizia kusudi umzalie matunda halelluyah
Kumbe nisipoifia torati
Sio mali ya Yesu na pia siwezi mzalia matunda huyo Yesu

Inaendeleaa.....

Comments

Yaliyopendwa zaidi

UMENUNULIWA

NJIA TANO ZA KUFANIKIWA