Posts

UTAMBUE NA UTAMKE UUNGU WAKO-Rapsodi ya uhakika Jumatatu 16 August

  Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16). M stari wetu wa ufunguzi si ahadi; ni sheria. Ni kama tu vile 2 Wakorintho 5:17. “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”     Huu na mstari wetu wa ufunguzi si ahadi za kutoka kwa Mungu; ni matamko ya kifalme toka kwa Mungu. Yule aliyezaliwa tena ni kiumbe kipya; anao uzima na asili ya Mungu. Kuwa umezaliwa tena, uhai wako wa kibinadamu ulimezwa na uzima na asili ya Mungu. Sasa, mwili wako unafunika aina mpya ya uzima ambao hauingiliki wala kufikiwa na maradhi au magonjwa. Mambo ya kale yamepita; tazama, mambo yote yamekuwa mapya! Kama haujui kuhusiana na uzima huu mpya, kamwe hautauweka katika matendo; utakuwa ukiishi maisha ya kibinadamu angali una uzima wa kiungu ndani yako. Jifunze kuuchochea uzima wa kiungu ndani yako, kwa kutamka na ...

UMENUNULIWA

Bwana Yesu Asifiwe!   Biblia inatufundisha jambo la msingi sana—kila aliyeokoka amenunuliwa. " Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu ." 1 Wakorintho 7:23 Hili ni suala la umiliki: Nani anakumiliki?   Kama tulinunuliwa, basi ni dhahiri kuwa kulikuwa na aliyehusika kukuuza , na kuna mwingine aliyekununua .  Hii pia inamaanisha wazi kuwa wewe si mali yako mwenyewe.  Fikiria gari— halijinunui lenyewe. Linahitaji mmiliki.  Vivyo hivyo, chochote kinachoweza kununuliwa, hakiwezi kujimiliki chenyewe.  Hili linabeba uzito mkubwa sana: Haijalishi umeokoka au hujaokoka—kila mtu yuko chini ya umiliki. Na ikiwa Mungu ndiye aliyekununua, basi kuna aliyekuuza. Na hapa ndipo tunaona ufahamu mdogo wa shetani:   Alimuuza mwanadamu pasipo kujua kuwa anapoteza kabisa haki ya umiliki Juu ya mwandamu!  Shetani alisaini mkataba huu alipomtumia Yuda kumsaliti Yesu—akidhani anashinda, kumbe anauza mali aliyokuwa anaimiliki.   Uthamani ...

KICHWA CHA KANISA

 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. ‭‭Wakolosai‬ 1:18‬ ‭SUV‬‬ Habari Mpendwa wa Mungu, Leo tujifunze kuhusu mwili wa Kristo, Mwili wa Kristo ndio kanisa lenyewe na kanisa ni mimi na wewe, Wewe hapo ni kanisa jinsi ulivo Kichwa cha kanisa ni Yesu mwenyewe kwahio wewe kama kanisa ni mwili tu ila kichwa ni Yesu Nini maana halisi ya Kichwa cha kanisa? Kichwa ndio kina macho,mdomo,pua,masikio na ubongo(akili) Huwezi kuona,kusikia,kunusa,kuongea,k ufikiri pasipo kua na kichwa Kama Yesu ndio kichwa cha kanisa basi kanisa haliwezi kufanya hayo mambo yote pasipo Yesu. Ili uweze kutembea katika utimilifu wa Kanisa yani uweze kuenenda kama kanisa Lazima uwe na uwezo wa kujua Yesu anawaza nini, Hili ndilo la Msingi. Mfano Wewe binafsi kila kitu unachofanya haukitamki kwa mdomo wako kua unakifanya bali unakiwaza ndo unakifanya. Mfano nataka kunywa maji Ili mguu uweze ku...

SIRI YA WOKOVU 3

 Inaendelea.. Warumi 7:14  Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Kwa maana twajua torati asilimyake ni ya rohoni Bali mimi ni mtu wa mwilini Warumi 7:5  Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. Hapa anasema tulipokua katika hali ya mwili Ikidhihirisha kuwa sasa hivo hatuko katika hali ya mwili Kwahio hapa sio expirience ya paulo ambayo anapitia akiwa ndani ya wokovu noo noo Ni expirence aliokua nayo kabla hajaokoka Ndio maana kule juu alisema tulipokua katika mwili akidhihirisha kua aliempokea Yesu hayuko katka mwili Afu anasema nmeuzwa chini ya dhambi Niulize tena Hatujaona mahali amesema tumeifia torati ili tuwe mali ya mwingine? Warumi 7:4  Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwin...

SIRI YA WOKOVU 2

Inaendelea,,, Warumi 7:5  Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.  Anasema tulipokuwa katika hali ya mwili Halleluyah kumbe saivi sipo katika hali yake ya mwili Paulo ametoboa siri yote hapaa Anasma tulipokua katika hali ya mwili Tamaa ya dhambii zilikuwako kwa sababu ya torati Kumbe kwanini kipindi hatujampokea Yesu tulikua tunatenda dhambi kwa fujo sana Kwasababa tamaa ya dhambi ilikuwako kwasababu ya torati Lakini sasa mimi sipo katika mwili kwahio ina maana tamaa ya dhambi haiwezi kuwako tena Inatoka wapi ? Heey Afu anasema hizo tamaa zilitenda dhambi katika viungo vyenu Kua makini anaongelea wakati ulipita sio wakati uliopo Anachomaanisha mtu aliemuamini Yesu hayupo mwilini Hivo tamaa za dhambi haziwezi kumtawala Ooh utasema mbona nmeokoka na tamaa bado zinanisumbua Haha ni kwasababu ulikua hujui ukweli huu ndo nakwambia ...

SIRI YA WOKOVU 1

 Warumi 7:1   Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai? Ndugu zangu hamjui ya kua sheria inamtawala mtu akiwa hai Warumi 7:2  Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Anasema mwanamke akiwa ameolewa na mwanaume kuna sheria inayowafunga Mwanamke huyu akienda kwa mme mwingine wakati mme wako bado yu hai basi atakua amevunja sheria Lakini mume anapokufa huyu mwanamke ile sheria haimfungi tena Sasa utaona jinsi sheria ilivofanya kazi kwamba bila kifo sheria ilimtawala mkee Warumi 7:3  Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine. Sasa mume akiwa hai Huyu mke akienda kwa mme mwingine ni mzinzi kwasababu ya ile sheria Lakini anapokufa mme a...

NJIA TANO ZA KUFANIKIWA

  Bwana asifiwe, Kila mtu anapenda kufanikiwa, lakini tatizo limekua ni namna gani ambavyo mtu unaweza kufanikiwa. Leo nmewaandalia njia tano ambazo wewe mkristo ukifuatilia lazima uone mafanikio. Unatakiwa ujue mambo haya kwanza kabla hujafikiria jinsi ya kufanikiwa Ni mapenzi ya MUNGU kuona wewe unafanikiwa 3 YOHANA 1:2 " Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kua na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo" Ni MUNGU pia anayekupa nguvu za kuweza kufanikiwa  KUMBUKUMBU LA TORATI 8:18 " Bali utamkumbuka BWANA ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo"  Baada ya kufahamu hayo sasa basi tutakwenda kuona ni vitu gani ambavo vinaweza kumfanya mkristo afanikiwe kwa kupitia mifano halisi kwenye neno la MUNGU.     1.  KUISHI VIZURI NA MUNGU Jinsi utakavoishi na kumpendeza MUNGU ndivo MUNGU atakapo kukubariki na kukuongeza zaidi na zaidi. ZABURI 1:1 "  Her...