UMENUNULIWA
Bwana Yesu Asifiwe! Biblia inatufundisha jambo la msingi sana—kila aliyeokoka amenunuliwa. " Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu ." 1 Wakorintho 7:23 Hili ni suala la umiliki: Nani anakumiliki? Kama tulinunuliwa, basi ni dhahiri kuwa kulikuwa na aliyehusika kukuuza , na kuna mwingine aliyekununua . Hii pia inamaanisha wazi kuwa wewe si mali yako mwenyewe. Fikiria gari— halijinunui lenyewe. Linahitaji mmiliki. Vivyo hivyo, chochote kinachoweza kununuliwa, hakiwezi kujimiliki chenyewe. Hili linabeba uzito mkubwa sana: Haijalishi umeokoka au hujaokoka—kila mtu yuko chini ya umiliki. Na ikiwa Mungu ndiye aliyekununua, basi kuna aliyekuuza. Na hapa ndipo tunaona ufahamu mdogo wa shetani: Alimuuza mwanadamu pasipo kujua kuwa anapoteza kabisa haki ya umiliki Juu ya mwandamu! Shetani alisaini mkataba huu alipomtumia Yuda kumsaliti Yesu—akidhani anashinda, kumbe anauza mali aliyokuwa anaimiliki. Uthamani ...