KICHWA CHA KANISA
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Wakolosai 1:18 SUV
Habari Mpendwa wa Mungu,
Leo tujifunze kuhusu mwili wa Kristo,
Mwili wa Kristo ndio kanisa lenyewe na kanisa ni mimi na wewe,
Wewe hapo ni kanisa jinsi ulivo
Kichwa cha kanisa ni Yesu mwenyewe kwahio wewe kama kanisa ni mwili tu ila kichwa ni Yesu
Nini maana halisi ya Kichwa cha kanisa?
Kichwa ndio kina macho,mdomo,pua,masikio na ubongo(akili)
Huwezi kuona,kusikia,kunusa,kuongea,k
Kama Yesu ndio kichwa cha kanisa basi kanisa haliwezi kufanya hayo mambo yote pasipo Yesu.
Ili uweze kutembea katika utimilifu wa Kanisa yani uweze kuenenda kama kanisa
Lazima uwe na uwezo wa kujua Yesu anawaza nini,
Hili ndilo la Msingi.
Mfano
Wewe binafsi kila kitu unachofanya haukitamki kwa mdomo wako kua unakifanya bali unakiwaza ndo unakifanya.
Mfano nataka kunywa maji
Ili mguu uweze kutembea niende mahali maji yalipo,hainihitaji niongee kwa sauti kua *nataka kunywa maji* ili mguu ujue kua unatakiwa kwenda kunywa maji
Ila nikiwaza tu mguu unapata taarifa ndipo unachukua hatua kwenda maji yalipo
Lakini pia kichwa hicho hicho ndo kinaongoza miguu na kukijulisha mahali maji yalipo
Maana akili ndo inatakiwa ikumbuke njia ya kwenda kuchukua maji.
Sasa basi kwa mfano huo tunaona kua wewe kama mwili wa Kristo usitegemee kusikia Yesu akiongea ili uweze kuchukua hatua bali unatakiwa ujue Yesu anawaza nini ili uweze kuchukua hatua,
Watu wengi husubiria Yesu aongee ili wachukue hatua pasipo kuelewa kua wanajichelewesha wanatakiwa wajue akili ya Yesu inawaza nini?
Swali la msingi
*nitajueje Yesu anawaza nini?*
Ili uweze kujua Yesu anawaza nini ili ufanye mapenzi yake yaani kama ni mwili Yesu akitaka kukaa wewe kama mwili ukae maana hatotangaza ninakaa ili uelewa ila atawaza wewe kama mwili unatakiwa kurespond, usiporespond ni kama tu ume paralyse
Njia pekee ni kusoma na kutafakari neno
Maana neno ndio Yesu mwenyewe ukitaka kujua tabia yake vitu anavofikiri soma neno ili uanze kufikiri kama yeye.
Tusome hii
Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
1 Wakorintho 2:16 SUV
Nia ya Bwana ni kile ambacho Bwana Yesu anataka kufanya,
Sasa kama Yesu ni Kichwa cha kanisa na wewe ni mwili wake lazima uwe na nia yake ili uweze kujua Yesu anataka ufanye nini.
Ubarikiwe kwa somo hili!!
Comments
Post a Comment