ROHO NA MWILI

 Mwanzo 1:26
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu
Hii lazima ikupe maswali kua Mungu anafananaje?

Biblia inatupa majibu kua Mungu anafananaje.

Yohana 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli


Biblia inasema Kua Mungu ni roho
Hivo basi Mungu akisema tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwasura yetu basi hapo tunajua kua Mungu anamfanya mtu ambae ni roho na yeye

Ila huyo mtu ambae ni Roho kuna dhumuni kuu aliloumbiwa

Aliumbwa ili atawale, Mungu baada ya kuumba kila kitu akataka mtawala na huyo mtawala alitaka afanane nae
Kwahio Mungu akamfanya mtu ambae ni Roho

Mwanzo 1:27
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake
Mwanaume na mwanamke
Hii ni siku moja
Kwahio mwanamke na mwanaume waliumbwa siku moja katika Roho
Na hakusema Roho moja awe msaidizi wa mwingine lakini wote kwa pamoja aliwaumba kwa ajili ya kutawala

Lakini usisahau kua walioumbwa kwa ajili ya kutawala ni wale wa Rohoni

Baada ya Mungu kuumuumba mwanamme na mwanamke katika Roho
Alifanya yafuatayo

Mwanzo 1:28
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Mungu akawabariki
Usisahau baraka hizi zinakwenda kwa mtu wa Rohoni
Akawaambia zaeni,mkaongezeke,wakatawale na mambo yote ya kimamlaka walipewa

Ila walipewa watu wa rohoni

Sasa katika Sura ya pili ya kitabu cha mwanzo tunaona sasa Mungu sasa akimuumba mtu katika mavumbi na huoni akisema tumfanye mtu kwa mfano wake maana huo haukua mfano wake

Mwanzo 2:7
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Ila Siku anapomuumba mtu katika mwili alimuumba mmoja tu ambae ni mwanaume
Ina maana sada roho ya mwanaume ilipata mwili tayari kwahio mwili ukakutana na Roho

Sasa utashangaa kuona Mungu maagizo aliyoyatoa kwa adamu pale alipokamilika katika mwili na Roho

Mwanzo 2:15
Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.


Mungu hakupoteza mda kuanza tena kubariki na mwili wa adamu
Chap chap akaupatia kazi
Akamuweka kwenye bustani afu akamwambia alime na aitunze

Lakini kama haitoshi Mungu akampa na masharti huyu mtu

Mwanzo 2:17
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Akamuonya usile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya maana siku atakayo kula hakika atakufa

Yani ile siku atakayokula lile tunda siku hio hio ndo atakufa.

Hii inaonyesha kwanza kua mtu wa Rohoni sio rahisi kumtamanisha uovu
Ila mwili ni dhaifu mahali popote panapohusisha jambo kimwili lazima kuwe na mipaka

Ndio maana Maagizo aliopewa mwanamke na mwanamme wakati wako rohoni ni tofauti na pale adamu alivokuja katika mwili

Roho iko radhi kutenda mema lakini mwili ndio unaosababisha udhaifu

Na Mungu kwa kujua hili akampa angalizo kabisa mtu wa mwilini lakini hatuoa angalizo kwa mtu wa Rohoni

Lakini pia tofauti nyingine ni hii
Vitu vyote huanzia rohoni kwanza ndio huja mwilini
Mungu alimuumba adam na hawa kwanza Rohoni ndio akaja kuumba mwilini

Na pia jambo la mwenzako likianza kudhihirika katika mwili haimaniishi kua lako halipo ila bado tu mda wake

Kumbuka adam na hawa kiroho waliumbwa siku moja lakini kimwili kila mtu aliumbwa siku yake

Hii inamaana baraka ya mtu ipo rohoni tayari inasubiria tu wakati wa kudhihirika

Ni kweli unaweza kupokea neno la kinabii siku moja na mwenzako la mwenzako likawahi kutokea kabla ya lako
Haimaanishi kwamba halipo
Bali mda wake bado
Ubarikiwe kwa somo hili
Amen

Comments

Yaliyopendwa zaidi

SIRI YA WOKOVU 1

UMENUNULIWA

NJIA TANO ZA KUFANIKIWA