Siri Ya Msalaba
Habari Mpendwa,
Leo tunaenda kujifunza siri iliojificha kwenye msalaba wa Yesu, ni tumaini langu kubwa utapata kitu cha kujifunza.
Yohana 3:14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
Jangwani Musa alimuinua nyoka
Ilikua ni kivuli cha Yesu, Lakini jiulize kwanini mwana wa Mungu Yesu Kristo alifananishwa na nyoka
Kwanini katika wanyama wote Mungu aliamua kumfananisha na Nyoka
Tunamjua Yesu kama mwana kondoo
Lakini kwanini hasa hapa anafananishwa na nyoka yule aliyekua muerevu pale bustanini?
Ebu tumia sekunde kazaa kutafakari siri hii
Mungu alitumia mnyama yule yule anaemuwakilisha shetani pale edeni
Kumfananisha na mwanae
Lazima nitafakari sifa za nyoka
Nyoka akikungata anaacha sumu ndani yako
Sumu kazi yake kuua
Na mnajua watu wote waliong'atwa na nyoka walienda kumuangalia nyoka aliinuliwa na Musa ndipo walipopona
Sasa kama yale yalikua kivuli cha Yesu
Na kivuli kile kilikua ukingatwa na nyoka unaenda kumuangalia nyoka alie inuliwa
Ina maana kinachoangaliwa lazima kifanane na kilichokung'ata
Maana nyoka kakung'ata basi muangalie nyoka
Kwahio namuangalia Yesu msalabani kwa sababu ya kitu kilichosababishwa na aliefanana na alie msalabani
Ni kitu gani hasa kilichokua kinafanana na Yesu pale msalabani ambacho kilikua kimetudhuru sisi wanadamu ndani yetu kukawa na sumu ambayo inaleta umauti
Najua wote tunajua kua ni dhambi
Lakini je Mungu kamfananisha mwanae Yesu Kristo na dhambi?
Kwahio Yesu akiwa msalabani alikua ni nani?
Hivi ndivo biblia inavosema Yesu alikuwa nani pale msalabani
2 Wakorintho 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Yeye asiyejua dhambi
Alimfanya kuwa dhambi
Kuna tofauti ya dhambi na mtenda dhambi
Yesu hakufanywa kua mtenda dhambi noo
Alifanywa kua dhambi yenyewe alivokuwa msalabani
Unazani Yesu alivokua analia pale bustanini ilikuwa ni kwasababu ya mateso ya msalaba noo
Kwake hilo halikujalisha
Ishu iliyokua ngumu kwake ni kufanyika kuwa dhambi
Maana alijua atakavofanyika kuwa dhambi tuu
Basi Mungu Baba hapo hapo atamuacha na ni kitu ambacho Yesu hakijawahi kutokea kwake kutenganishwa na Baba yake
Ndio maana pale msalabani akalia Eloi Eloi lama sabaktani
Yani Mungu wangu mbona umeniacha?
Ni sehemu hio pekee Yesu aliliaa mbele za Mungu sehemu zote alivumilia lakini sio kuachwa na Baba
Mungu alimuacha kwasababu alikuwa dhambi
Kwahio sio Yesu tunaemjua anasulubiwa bali ni dhambi inasulubiwa
Ebu rudi kule jangwani
Mtu aliengatwa na nyoka
Unazani habari njema kwake ilikua ni hipi?
Habari njema ilikuwa ni kuambiwa kua tiba ipo
Na tiba hio ndio kumuangalia Nyoka
Kwahio unapomuona Yesu msalabani lazima ujue pale alifanyika kuwa dhambi
Kwahio pale ndo ufunuo halisi wa kwanini alifananishwa na nyoka aliyekua jangwani
Hivo Yesu pale msalabani moja ya kazi aliyoifanya
Nasema moja kwasababu msalaba umeshughulikia maeneo kadha wa kadha
Lakini moja ya kazi kuu ni kutoa tiba ya dhambi
Unachotakiwa ni kuangalia (kuamini) tu msalaba
Hivo nyoka kwa neno hili alifananishwa na dhambi na ile sumu sasa ndio iletayo mauti na ndio matokeo ya dhambi.
Ubarikiwe kwa somo hili.
Comments
Post a Comment