SIRI YA WOKOVU 2
Inaendelea,,,
Warumi 7:5
Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.
Anasema tulipokuwa katika hali ya mwili
Halleluyah kumbe saivi sipo katika hali yake ya mwili
Paulo ametoboa siri yote hapaa
Anasma tulipokua katika hali ya mwili
Tamaa ya dhambii zilikuwako kwa sababu ya torati
Kumbe kwanini kipindi hatujampokea Yesu tulikua tunatenda dhambi kwa fujo sana
Kwasababa tamaa ya dhambi ilikuwako kwasababu ya torati
Lakini sasa mimi sipo katika mwili kwahio ina maana tamaa ya dhambi haiwezi kuwako tena
Inatoka wapi ? Heey
Afu anasema hizo tamaa zilitenda dhambi katika viungo vyenu
Kua makini anaongelea wakati ulipita sio wakati uliopo
Anachomaanisha mtu aliemuamini Yesu hayupo mwilini
Hivo tamaa za dhambi haziwezi kumtawala
Ooh utasema mbona nmeokoka na tamaa bado zinanisumbua
Haha ni kwasababu ulikua hujui ukweli huu ndo nakwambia sasa
Ni sawa na mtoto alieachiwa urithi lakini hajui kua yeye ni tajiri hivo anaweza kuishi hata maisha ya kimasikini ndivo wengi wanavoishi
Ndio maana paulo huyo huyo akasema mtoto mdogo hata kama ana urithi mkubwa akiwa mtoto bado ataishi kama mtumwa
Wengi wanazani kulijua neno ndio kukua kiroho
Lakini biblia inasema watoto wadogo msitende dhambi
Na hata mkitenda yupo muombezi kwa Baba
Kwanini hakusema watu wazima
Kwasababu ni mtoto tu katika Roho anaweza kutenda dhambi
Lakini ukija kugundua siri hii ya wokovu
Utashangaa na kujiuliza kua ni nani amelidanganya kanisa kua mtu hawezi kua mkamilifu
Ni ukweli unaotisha
Warumi 7:6
Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.
Tumefunguliwa katika toratii nmebold kabisa muionee vizuri
Yani kumbe mtu alieishikilia torati hasaa yupo kwenye kifungo?
Tumeifia ile hali iliyokua inatupinga
Ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya Roho
Si katika hali ya zamani ya andiko
Warumi 7:7
Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
Katika hayo yote najua utaanza kupata wasiwasi kuhusu torati na kuona kua ni mbaya
Ndio maana neno likasema
Basi tusemeje
Torati ni dhambi ?
La hasha wala sio dhambi
Lakini nisingejua kutamani kama torati isingesema usitamani?
Unajua mfano ukianza kufundisha acha uzinzi
Hehe ujue kuna watu walikua wameshasahau habari za uzinzi wanakaribia kupona kwahio ulivosema acha uzinzi onhoo ni kama umemkumbusha
Na hii ni mbinu ya kuishinda dhambi usiipe attention
Sasa torati sio dhambi ila dhambi inakua kama imepata fursa pale torati inapokua
Ile dhambi inakushawishi kutenda
Warumi 7:8
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
Sasa nikuulize swali tokea tumeanza je hapa paulo anajiongelea yeye ambaye ameokoka au yeye ambaye alikua kabla hajaokoka?
Je yeye aliyeokoka ameifia torati au hajaifia ?
Kwahio anaposema
Warumi 7:8
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
Ina maana anakupa historia ya maisha yake kabla hajaokoka sindio kwasababu yeye aliyeokoka ameifia dhambi kwahio hata haya hayawezi kua yanamhusu
Hivo anasema lakini dhambi ilipata(wakati uliopita) nafasi kwa ile amri yani torati
Ikafanya ndani yangu namna ya kutamani
Afu anasema dhambi bila sheria imekufa
Wewe unazani kama pale bustanini kungekua hamna sheria ya tunda la ujuzi wa mema na mabaya unazani leo kungekua na dhambi
Ndio maana Mungu anasisitiza kuhusu kuifia torati
Warumi 7:9
Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.
Anaendelea kusema kua alikua hai hapo kwanza bila sheria lakini ilipokuja torati dhambi ilihuika nami nikafa
Warumi 7:11
Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua.
Bado anaongelea kwa habari ya mtu ambaye hajaifia torati
Jinsi anavoteseka
Warumi 7:12
Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.
Anatetea kua torati kama torati ni takatifu
Na ya haki na ni njema kabisa
Sasa anaendelea na anafika mahali ambapo kanisa limekua likitafasiri vibaya
Warumi 7:13
Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.
Sasa anasema je ile iliyo njema ilikua mauti kwangu mimi
Angalia kwa makini ametumia wakati uliopita
Ntaendelea kusisitizia hapo
Akasema hapana haikua mauti kwako
Ila ili dhambi ionekane kua dhambi iliyumia ile njema
Yani usiibe ukiiba basi unaona effect za kuiba zilivo mbaya hivo inafanya ile torati kua safi kwa maana inafanya kile kibaya kionekana kibayaa
Inaendeleaa.....
Comments
Post a Comment