SIRI YA WOKOVU 3

 Inaendelea..

Warumi 7:14

 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

Kwa maana twajua torati asilimyake ni ya rohoni
Bali mimi ni mtu wa mwilini


Warumi 7:5 

Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.


Hapa anasema tulipokua katika hali ya mwili
Ikidhihirisha kuwa sasa hivo hatuko katika hali ya mwili

Kwahio hapa sio expirience ya paulo ambayo anapitia akiwa ndani ya wokovu noo noo
Ni expirence aliokua nayo kabla hajaokoka

Ndio maana kule juu alisema tulipokua katika mwili akidhihirisha kua aliempokea Yesu hayuko katka mwili

Afu anasema nmeuzwa chini ya dhambi

Niulize tena
Hatujaona mahali amesema tumeifia torati ili tuwe mali ya mwingine?

Warumi 7:4 

Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.


Hapa alisema kadhalika ndugu zangu mmeifa torati kwa njia ya mwili wa Kristo mpate kua mali ya Mwingine
Warumi 7:14 

Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.


Hapa anasema nmeuzwa chini ya dhambi
Utagundua hapa anaongelea kwa habari ya kipindi ambacho bado hajampokea Yesu

Kua hapa haongelei maisha ya Mkristo aliyeokoka bali mtu ambae hajaokoka

Warumi 7:15 

Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.


Huyu mtu ambaye anatenda hivo ni mtu ambaye hajaokoka sio wewe ulioifia torati


Ooh mbona nahisi kama hili neno linaniongelea mimi kabisa
Mbona vitu navofanya sivitaki
Well ulikua hujui tu ila sasa nmekupa ukweli huu anza kukiri sawa sawa na neno linavosema
Ni sawa na mtu anaeumwa
Afu neno linasema hauumwi unaamini nini?
Una amini hisia za mwili wako au neno

Wewe upo rohoni hata kama unajihisi haupo hizo ni hisia zako lakini neno linasema tuliofia torati hatupo katika mwili

Kwahio acha hizi habari za kukiri hili neno vibaya

Nmechagua kuamini neno la Mungu nasio hali au mazingira yangu

Neno la Mungu ni kioo
Nikilisoma najiona mimi nilivo

Sisahau kile nilichokiona kwenye neno
Maana nikisahau ni sawa na mtu anaejiangalia kwenye kioo afu akiondoka anasahau sura yake ikoje

Kama neno ni kioo ukiangalia unajiona
Neno linavosema wewe upo rohoni ujue neno linakuonyesha uhalisia wako uliokua huujui

Warumi 7:17 

Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

 
Mkristo ulieokoka unaweza kuchukua hili neno nakusema eti sio mimi ni dhambi ndani yangu
Dhambi gani?
 Yesu alifanyika kua dhambi hivo dhambi ilisulubiwa msalabani
Ni ukosefu wa maarifa ya kimungu kujiita kuwa yeye ni mwenye dhambi

Mkristo anaweza kutenda dhambi kwa kutaka
Lakini haimaanishi yeye ni mwenye dhambi

Kibiblia mwenye dhambi ni yule ambaye hajampokea Yesu

Warumi 7:24 

Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

 Ooh paulo ashukuriwe Yesu mwokozi alikua kutuokoa na mwili huu wa mauti
Ndio maana mstari unaofuata anasema

Warumi 7:25 

Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.

 
Anamshukuru Mungu wa Bwana Yesu kwasababu ya wokovu aliolutea


Ubarikiwe kwa somo hili!!

Comments

Yaliyopendwa zaidi

SIRI YA WOKOVU 1

UMENUNULIWA

NJIA TANO ZA KUFANIKIWA