UTAMBUE NA UTAMKE UUNGU WAKO-Rapsodi ya uhakika Jumatatu 16 August

 

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
(Yohana 3:16).

Mstari wetu wa ufunguzi si ahadi; ni sheria. Ni kama tu vile 2 Wakorintho 5:17. “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” 

 Huu na mstari wetu wa ufunguzi si ahadi za kutoka kwa Mungu; ni matamko ya kifalme toka kwa Mungu.
Yule aliyezaliwa tena ni kiumbe kipya; anao uzima na asili ya Mungu. Kuwa umezaliwa tena, uhai wako wa kibinadamu ulimezwa na uzima na asili ya
Mungu. Sasa, mwili wako unafunika aina mpya ya uzima ambao hauingiliki wala kufikiwa na maradhi au magonjwa. Mambo ya kale yamepita; tazama, mambo yote yamekuwa mapya! Kama haujui kuhusiana na uzima huu mpya, kamwe hautauweka katika matendo; utakuwa ukiishi maisha ya kibinadamu angali una uzima wa kiungu ndani yako.
Jifunze kuuchochea uzima wa kiungu ndani yako, kwa kutamka na kujibinafsisha maneno ya Mungu.
Kumbuka, miujiza mikuu kuliko yote hutendeka na
maneno. Ninatamani uelewe nguvu na nishati ya maneno yako! Biblia inasema, “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa...” (Isaya 33:24).
Kwanini? Ni kwasababu, wameutambua na kuukubali uungu wao.
Biblia inasema katika 2 Petro 1:4, “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu....” Wewe ni mshirika wa kundi la miungu; watokea juu; asili yako ni ya kiungu. Ndio maana Yesu alisema, ‘Je! Haikuandikwa katika sharia yenu
“Nimesema ndinyi miungu?” (Yohana 10:34). Utambue na kuutamka uungu wako; jizoeze kuuishi. Biblia inasema kuwasiliana, udhihirisho wa kila siku wa imani yako, huwa fanisi pale unapotambua na kutamka wewe ni nani ndani ya Kristo (Filimono 1:6).
Haleluya!

 

SALA

Ninakushukuru, Baba mwenye haki, kwa uzima wako ndani yangu; mimi ni wa kiungu, nimezaliwa kutawala na kushinda katika dunia hii! Maisha yangu ni ushuhuda wa neema, utukufu, na ukuu wako. Nimebarikiwa na mimi ni msambazaji wa baraka na wema wako, katika Jina la Yesu. Amina.
 

Comments

Yaliyopendwa zaidi

SIRI YA WOKOVU 1

UMENUNULIWA

NJIA TANO ZA KUFANIKIWA